Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;
Nehemia 9:3 - Swahili Revised Union Version Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha Torati ya BWANA, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama na kumwabudu BWANA, Mungu wao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Biblia Habari Njema - BHND Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Neno: Bibilia Takatifu Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma katika kile Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, kwa muda wa robo siku, na wakatumia robo nyingine kwa kuungama dhambi na kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Neno: Maandiko Matakatifu Wakasimama pale walipokuwa, wakasoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Torati ya bwana Mwenyezi Mungu wao kwa muda wa robo siku, na wakatumia robo nyingine kwa kuungama dhambi na kumwabudu bwana Mwenyezi Mungu wao. BIBLIA KISWAHILI Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha Torati ya BWANA, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama na kumwabudu BWANA, Mungu wao. |
Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;