Na kusanyiko lote wakafanya shauri kufanya sikukuu siku saba nyingine; wakafanya sikukuu siku saba nyingine kwa furaha.
Nehemia 8:13 - Swahili Revised Union Version Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababu za watu wote, na makuhani, na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kujifunza maneno ya torati. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kesho yake, wakuu wa koo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, ili kujifunza sheria. Biblia Habari Njema - BHND Kesho yake, wakuu wa koo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, ili kujifunza sheria. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kesho yake, wakuu wa koo pamoja na makuhani na Walawi wakakusanyika kwa Ezra mwandishi, ili kujifunza sheria. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa jamaa zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi ili wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Torati. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa mbari zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi ili wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Torati. BIBLIA KISWAHILI Hata siku ya pili wakuu wa mbari za mababu za watu wote, na makuhani, na Walawi, wakamkusanyikia Ezra, mwandishi, ili wapate kujifunza maneno ya torati. |
Na kusanyiko lote wakafanya shauri kufanya sikukuu siku saba nyingine; wakafanya sikukuu siku saba nyingine kwa furaha.
Na watu wote wakaenda zao kula na kunywa, na kuwapelekea watu sehemu, na kufanya furaha nyingi, kwa sababu walikuwa wameyafahamu maneno yale waliyohubiriwa.
Wakaona ya kuwa imeandikwa katika torati, jinsi BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa, ya kwamba wana wa Israeli wakae katika vibanda, katika sikukuu ya mwezi wa saba;
Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia Maandiko?
Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na walinzi wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,