Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Nehemia 7:73 - Swahili Revised Union Version Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, makuhani, Walawi, walinzi wa hekalu, waimbaji, baadhi ya watu wengine, watumishi wa hekalu na watu wote wa Israeli, wakaishi katika miji yao. Biblia Habari Njema - BHND Basi, makuhani, Walawi, walinzi wa hekalu, waimbaji, baadhi ya watu wengine, watumishi wa hekalu na watu wote wa Israeli, wakaishi katika miji yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, makuhani, Walawi, walinzi wa hekalu, waimbaji, baadhi ya watu wengine, watumishi wa hekalu na watu wote wa Israeli, wakaishi katika miji yao. Neno: Bibilia Takatifu Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe. Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao, Neno: Maandiko Matakatifu Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe. Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao, BIBLIA KISWAHILI Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao. |
Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.
Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu.
Basi hawa ndio viongozi wa jimbo waliokaa Yerusalemu; ila mijini mwa Yuda wakakaa kila mtu katika milki yake mijini mwao, yaani, Israeli, makuhani, na Walawi, na Wanethini, wazawa wa watumishi wa Sulemani.
Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.