na masufuria, na majembe, na mabeseni; hata vyombo hivyo vyote, Huramu alivyomfanyia mfalme Sulemani, katika nyumba ya BWANA, vyote vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.
Nehemia 7:70 - Swahili Revised Union Version Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni, za dhahabu elfu moja, na mabeseni hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530. Biblia Habari Njema - BHND Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530. Neno: Bibilia Takatifu Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni elfu moja za dhahabu, mabakuli hamsini, na mavazi mia tano na thelathini ya makuhani. Neno: Maandiko Matakatifu Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. BIBLIA KISWAHILI Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni, za dhahabu elfu moja, na mabeseni hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini. |
na masufuria, na majembe, na mabeseni; hata vyombo hivyo vyote, Huramu alivyomfanyia mfalme Sulemani, katika nyumba ya BWANA, vyote vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.
na nyuma, na mabakuli, na vikombe vya dhahabu safi; na kwa matasa ya dhahabu, kwa uzani kwa kila tasa; na kwa matasa ya fedha, kwa uzani kwa kila tasa;
Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni. Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu;
Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu.
Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.
Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili.
Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.
Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu yeyote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu.
Navyo vikombe, na vyombo vya kutolea majivu, na mabakuli, na masufuria, na vinara, na miiko, na vyetezo, vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.