Basi, viongozi wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale tisa wakae mijini.
Nehemia 7:4 - Swahili Revised Union Version Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa wachache, na nyumba zilikuwa hazijajengwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mji wa Yerusalemu ulikuwa mpana na mkubwa, lakini wakazi wake walikuwa wachache na nyumba zilikuwa hazijajengwa. Biblia Habari Njema - BHND Mji wa Yerusalemu ulikuwa mpana na mkubwa, lakini wakazi wake walikuwa wachache na nyumba zilikuwa hazijajengwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mji wa Yerusalemu ulikuwa mpana na mkubwa, lakini wakazi wake walikuwa wachache na nyumba zilikuwa hazijajengwa. Neno: Bibilia Takatifu Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. Neno: Maandiko Matakatifu Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. BIBLIA KISWAHILI Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa wachache, na nyumba zilikuwa hazijajengwa. |
Basi, viongozi wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale tisa wakae mijini.
Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejesha njia za kukaa.