Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.
Nehemia 5:19 - Swahili Revised Union Version Unikumbuke, Ee Mungu wangu, kwa mema, wote niliowatendea watu hawa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa, ee Mungu wangu, kumbuka wema wangu wote niliowatendea watu hawa. Biblia Habari Njema - BHND Sasa, ee Mungu wangu, kumbuka wema wangu wote niliowatendea watu hawa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa, ee Mungu wangu, kumbuka wema wangu wote niliowatendea watu hawa. Neno: Bibilia Takatifu Unikumbuke kwa fadhili, Ee Mungu wangu, kwa yote niliyofanya kwa ajili ya watu hawa. Neno: Maandiko Matakatifu Unikumbuke kwa fadhili, Ee Mungu wangu, kwa yote niliyofanya kwa ajili ya watu hawa. BIBLIA KISWAHILI Unikumbuke, Ee Mungu wangu, kwa mema, yote niliowatendea watu hawa. |
Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.
Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Unikumbukie hayo, Ee Mungu wangu, wala usifute fadhili zangu nilizozitenda kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, na kwa taratibu zake.
Kisha nikawaamuru Walawi wajitakase, nao waje kuyalinda malango, ili kuitakasa siku ya sabato. Unikumbukie hayo nayo, Ee Mungu wangu, ukaniachilie sawasawa na wingi wa rehema zako.
na kuleta kwa kuni na malimbuko, katika nyakati zilizoamriwa. Nikumbuke, Ee Mungu wangu, ili unitendee mema.
Ee BWANA, unikumbuke mimi, Kwa kibali ulicho nacho kwa watu wako. Unijie kwa wokovu wako,
Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa angaa kikombe cha maji baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.
Kwa kuwa yeyote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.