Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, niliamuru milango ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wowote siku ya sabato.
Nehemia 13:20 - Swahili Revised Union Version Basi wenye biashara na wachuuzi wa bidhaa za kila namna wakalala nje ya Yerusalemu mara moja au mbili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mara mbili au tatu hivi wafanyabiashara waliokuwa wakiuza bidhaa za aina mbalimbali iliwabidi kulala nje ya mji. Biblia Habari Njema - BHND Mara mbili au tatu hivi wafanyabiashara waliokuwa wakiuza bidhaa za aina mbalimbali iliwabidi kulala nje ya mji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mara mbili au tatu hivi wafanyabiashara waliokuwa wakiuza bidhaa za aina mbalimbali iliwabidi kulala nje ya mji. Neno: Bibilia Takatifu Mara moja au mbili wachuuzi na wauzaji wa bidhaa za aina zote walilala usiku nje ya mji wa Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Mara moja au mbili wachuuzi na wauzaji wa bidhaa za aina zote walilala usiku nje ya mji wa Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Basi wenye biashara na wachuuzi wa bidhaa za kila namna wakalala nje ya Yerusalemu mara moja au mbili. |
Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, niliamuru milango ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wowote siku ya sabato.
Ndipo nikawashuhudia, nikawaambia, Mbona mnalala nje ya mji? Mkitenda hivi tena, nitawakamata. Tangu wakati ule hawakuja tena siku ya sabato.