Hushai akaendelea kusema, Unamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.
Nahumu 2:12 - Swahili Revised Union Version Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwakamatia majike wake mawindo, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza nyama iliyoraruliwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha, akawakamatia simba majike mawindo yao; ameyajaza mapango yake mawindo, na makao yake mapande ya nyama. Biblia Habari Njema - BHND Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha, akawakamatia simba majike mawindo yao; ameyajaza mapango yake mawindo, na makao yake mapande ya nyama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Simba dume amewararulia watoto wake nyama ya kutosha, akawakamatia simba majike mawindo yao; ameyajaza mapango yake mawindo, na makao yake mapande ya nyama. Neno: Bibilia Takatifu Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake, alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake, akijaza makao yake kwa alivyoua na mapango yake kwa mawindo. Neno: Maandiko Matakatifu Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake, alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake, akijaza makao yake kwa alivyoua na mapango yake kwa mawindo. BIBLIA KISWAHILI Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwakamatia majike wake mawindo, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza nyama iliyoraruliwa. |
Hushai akaendelea kusema, Unamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.
Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amenila, ameniponda, amenifanya kuwa chombo kitupu; amenimeza kama joka, amelijaza tumbo lake vitu vyangu vya anasa; amenitupa
Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wanasimba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwanasimba, wala hapana aliyewatia hofu?
Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.
Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.