Ahimidiwe Mungu Aliye Juu Sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Mwanzo 9:26 - Swahili Revised Union Version Akasema, Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena akasema, “Shemu na abarikiwe na Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kanaani na awe mtumwa wake. Biblia Habari Njema - BHND Tena akasema, “Shemu na abarikiwe na Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kanaani na awe mtumwa wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena akasema, “Shemu na abarikiwe na Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kanaani na awe mtumwa wake. Neno: Bibilia Takatifu Pia akasema, “Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Shemu! Kanaani na awe mtumwa wa Shemu. Neno: Maandiko Matakatifu Pia akasema, “Abarikiwe bwana, Mungu wa Shemu! Kanaani na awe mtumwa wa Shemu. BIBLIA KISWAHILI Akasema, Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake. |
Ahimidiwe Mungu Aliye Juu Sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. BWANA akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Alaaniwe yeyote yule atakayekulaani, Na abarikiwe yeyote yule atakayekubariki.
Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu?
Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.
watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.
ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake.
Lakini sasa wanaitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
Basi sasa mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.
Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepata nguvu, ndipo walipowatia hao Wakanaani katika kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa.