wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yoyote.
Mwanzo 7:15 - Swahili Revised Union Version Waliingia katika safina alimokuwa Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waliingia ndani ya safina pamoja na Noa wiliwawili wa kila aina ya viumbe hai. Biblia Habari Njema - BHND Waliingia ndani ya safina pamoja na Noa wiliwawili wa kila aina ya viumbe hai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waliingia ndani ya safina pamoja na Noa wiliwawili wa kila aina ya viumbe hai. Neno: Bibilia Takatifu Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai vikaja kwa Nuhu viwili viwili, vikaingia katika safina. Neno: Maandiko Matakatifu Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Nuhu viwili viwili, vikaingia katika safina. BIBLIA KISWAHILI Waliingia katika safina alimokuwa Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. |
wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yoyote.
Na walioingia, waliingia wa kike na wa kiume, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia.
wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kike na wa kiume, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.
Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng'ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.