Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
Mwanzo 7:10 - Swahili Revised Union Version Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaanza kuifunika nchi. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaanza kuifunika nchi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaanza kuifunika nchi. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia. BIBLIA KISWAHILI Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. |
Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arubaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kike na wa kiume, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.
Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.