Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko.
Mwanzo 42:3 - Swahili Revised Union Version Basi ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri ili wanunue nafaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo ndugu kumi wa Yosefu wakaenda Misri kununua nafaka. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo ndugu kumi wa Yosefu wakaenda Misri kununua nafaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo ndugu kumi wa Yosefu wakaenda Misri kununua nafaka. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo ndugu kumi wa Yusufu wakateremka huko Misri kununua nafaka. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo wale ndugu kumi wa Yusufu, wakateremka huko Misri kununua nafaka. BIBLIA KISWAHILI Basi ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri ili wanunue nafaka. |
Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko.
Akasema, Angalia, nimesikia ya kuwa kuna nafaka Misri; shukeni huko mkatununulie chakula, tupate kuishi wala tusife.
Lakini Benyamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumpeleka pamoja na ndugu zake, maana alisema, Mabaya yasimpate.
Wana wa Israeli wakaja wanunue chakula miongoni mwao waliokuja, kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya Kanaani.