Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mwanzo 40:11 - Swahili Revised Union Version

Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mkononi mwangu nilikuwa na kikombe cha Farao, basi, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe hicho, nikampa Farao.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mkononi mwangu nilikuwa na kikombe cha Farao, basi, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe hicho, nikampa Farao.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mkononi mwangu nilikuwa na kikombe cha Farao, basi, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe hicho, nikampa Farao.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu. Nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, na nikaweka kikombe mkononi mwake.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, na nikaweka kikombe mkononi mwake.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mwanzo 40:11
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.


Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana kwamba unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva.


Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu.


Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake.


Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.


na chakula cha mezani pake, na maofisa wake walivyokaa, na kuhudumu kwao wahudumu wake, na mavazi yao, na wanyweshaji wake, na sadaka zake za kuteketezwa ambazo alizitoa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.


na vyakula vya mezani mwake, na kikao cha maofisa wake, na huduma ya watumishi wake na mavazi yao; pia wanyweshaji wake na mavazi yao; na daraja yake ya kupandia mpaka nyumba ya BWANA; roho yake ilizimia.


Ee Bwana, nakusihi, litege sikio lako, uyasikilize maombi ya mtumishi wako, na maombi ya watumishi wako, wanaofurahi kulicha jina lako; nakuomba sana; unifanikishe mimi, mtumishi wako, leo, ukanijalie rehema mbele ya mtu huyu. (Maana, nilikuwa mnyweshaji wa mfalme).


Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na vyombo vyako vitafurika divai mpya.


Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;