Mwanzo 4:13 - Swahili Revised Union Version Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imeniwia kubwa, haichukuliki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kaini akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Adhabu yangu ni kubwa mno; siwezi kuistahimili. Biblia Habari Njema - BHND Kaini akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Adhabu yangu ni kubwa mno; siwezi kuistahimili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kaini akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Adhabu yangu ni kubwa mno; siwezi kuistahimili. Neno: Bibilia Takatifu Kaini akamwambia Mwenyezi Mungu, “Adhabu yangu ni zaidi ya ninavyoweza kustahimili. Neno: Maandiko Matakatifu Kaini akamwambia bwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. BIBLIA KISWAHILI Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imeniwia kubwa, haichukuliki. |
Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao.
Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
Wanadamu wakaunguzwa na joto kali, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.