Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani.
Mwanzo 39:22 - Swahili Revised Union Version Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliokuwemo gerezani; na yote yaliyofanywa humo, yeye ndiye aliyeyafanya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo mkuu wa gereza alimweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa wote humo gerezani; kila kitu kilichofanyika humo kilifanywa kwa mamlaka yake. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo mkuu wa gereza alimweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa wote humo gerezani; kila kitu kilichofanyika humo kilifanywa kwa mamlaka yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo mkuu wa gereza alimweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa wote humo gerezani; kila kitu kilichofanyika humo kilifanywa kwa mamlaka yake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yusufu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yusufu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani. BIBLIA KISWAHILI Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliokuwemo gerezani; na yote yaliyofanywa humo, yeye ndiye aliyeyafanya. |
Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali wafungwa wa mfalme walimokuwa wamefungiwa, naye akawa humo gerezani.
Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?
Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau.