Mwanzo 32:22 - Swahili Revised Union Version Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiku huohuo Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wajakazi wake wawili na watoto wake kumi na mmoja, akapita kivuko cha Yaboki. Biblia Habari Njema - BHND Usiku huohuo Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wajakazi wake wawili na watoto wake kumi na mmoja, akapita kivuko cha Yaboki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiku huohuo Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wajakazi wake wawili na watoto wake kumi na mmoja, akapita kivuko cha Yaboki. Neno: Bibilia Takatifu Usiku ule Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wajakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Mto Yaboki. Neno: Maandiko Matakatifu Usiku ule Yakobo akaamka akawachukua wake zake wawili, watumishi wake wawili wa kike na wanawe kumi na mmoja na akavuka kivuko cha Yaboki. BIBLIA KISWAHILI Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. |
Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
upande wote wa mto wa Yaboki, na miji ya nchi ile ya milimani, na kila mahali alipotukataza BWANA, Mungu wetu.
Na Wareubeni na Wagadi niliwapa tokea Gileadi mpaka bonde la Arnoni, katikati ya bonde, na mpaka wake; mpaka mto wa Yaboki, nao ni mpaka wa wana wa Amoni;
Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hadi kuufikia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni;
Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu hao wajumbe wa Yeftha, “Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo walipokwea wakitoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena kwa amani.”