Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Abrahamu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Abrahamu; naye akaviita majina kufuata majina aliyoviita babaye.
Mwanzo 26:19 - Swahili Revised Union Version Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini watumishi wa Isaka walipochimba katika lile bonde na kupata kisima cha maji yanayobubujika, Biblia Habari Njema - BHND Lakini watumishi wa Isaka walipochimba katika lile bonde na kupata kisima cha maji yanayobubujika, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini watumishi wa Isaka walipochimba katika lile bonde na kupata kisima cha maji yanayobubujika, Neno: Bibilia Takatifu Watumishi wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakagundua huko kisima chenye maji safi. Neno: Maandiko Matakatifu Watumishi wa Isaka wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. BIBLIA KISWAHILI Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. |
Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Abrahamu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Abrahamu; naye akaviita majina kufuata majina aliyoviita babaye.
Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.
Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu, Kisima cha maji yaliyo hai, Vijito vya Lebanoni viendavyo kasi.
Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.