Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Mwanzo 21:6 - Swahili Revised Union Version Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye Sara akasema, “Mungu amenipatia kicheko; yeyote atakayesikia habari hizi, atacheka pamoja nami.” Biblia Habari Njema - BHND Naye Sara akasema, “Mungu amenipatia kicheko; yeyote atakayesikia habari hizi, atacheka pamoja nami.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye Sara akasema, “Mungu amenipatia kicheko; yeyote atakayesikia habari hizi, atacheka pamoja nami.” Neno: Bibilia Takatifu Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, na kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” Neno: Maandiko Matakatifu Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” BIBLIA KISWAHILI Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. |
Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia moja, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu.
Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.
Ndipo utasema moyoni mwako, Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami niko peke yangu, nimehamishwa, ninatangatanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, niliachwa peke yangu; hawa je! Walikuwa wapi?
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na uchungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Na alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari, akisema, Umezaliwa mtoto wa kiume; na kumfurahisha sana.
Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye.
Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
Akasema, Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba BWANA.