Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.
Mwanzo 21:34 - Swahili Revised Union Version Abrahamu akaishi kama mgeni kwa Wafilisti siku nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abrahamu alikaa katika nchi ya Wafilisti muda mrefu. Biblia Habari Njema - BHND Abrahamu alikaa katika nchi ya Wafilisti muda mrefu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abrahamu alikaa katika nchi ya Wafilisti muda mrefu. Neno: Bibilia Takatifu Naye Ibrahimu akakaa nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu. Neno: Maandiko Matakatifu Naye Ibrahimu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu. BIBLIA KISWAHILI Abrahamu akaishi kama mgeni kwa Wafilisti siku nyingi. |
Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.
Basi Abrahamu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Kwani sisi tu wageni na wapitaji mbele zako, kama walivyokuwa baba zetu wote; siku zetu duniani ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kuishi.
Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.
Hawa wote wakafa katika imani, walikuwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.