Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Mwanzo 11:32 - Swahili Revised Union Version Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205. Biblia Habari Njema - BHND Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205. Neno: Bibilia Takatifu Tera aliishi miaka mia mbili na mitano (205), akafa huko Harani. Neno: Maandiko Matakatifu Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205. BIBLIA KISWAHILI Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani. |
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha;
Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Je! Miungu ya mataifa wale, ambao baba zangu waliwaangamiza, imewaokoa? Yaani, Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari?
Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia moja na arubaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hadi kizazi cha nne.
Je! Miungu ya mataifa, ambao baba zangu waliwaangamiza, wamewaokoa? Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari?