Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Mwanzo 11:30 - Swahili Revised Union Version Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa. Biblia Habari Njema - BHND Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa. Neno: Bibilia Takatifu Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. Neno: Maandiko Matakatifu Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. BIBLIA KISWAHILI Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. |
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.
Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto wa kiume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;
Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.
naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto.
lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amemfunga tumbo.