Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
Mwanzo 11:1 - Swahili Revised Union Version Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale. Biblia Habari Njema - BHND Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwanza, watu wote duniani walikuwa na lugha moja na walitumia maneno yaleyale. Neno: Bibilia Takatifu Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. BIBLIA KISWAHILI Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. |
Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia BWANA wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa jua.
Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la BWANA, wamtumikie kwa nia moja.
Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.