Mhubiri 4:7 - Swahili Revised Union Version Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani. Biblia Habari Njema - BHND Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani. Neno: Bibilia Takatifu Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua: Neno: Maandiko Matakatifu Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua: BIBLIA KISWAHILI Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. |
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.