Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
Mhubiri 2:4 - Swahili Revised Union Version Nikajifanyia mambo makuu; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilifanya mambo makuu: Nilijenga majumba na kujilimia mashamba ya mizabibu. Biblia Habari Njema - BHND Nilifanya mambo makuu: Nilijenga majumba na kujilimia mashamba ya mizabibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilifanya mambo makuu: nilijenga majumba na kujilimia mashamba ya mizabibu. Neno: Bibilia Takatifu Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. Neno: Maandiko Matakatifu Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. BIBLIA KISWAHILI Nikajifanyia mambo makuu; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu; |
Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
Huyo Absalomu alipokuwa yu hai alikuwa ameitwaa na kujiinulia ile nguzo iliyoko bondeni mwa mfalme; kwa maana alisema, Mimi sina mtoto wa kuliendeleza jina langu; akaiita hiyo nguzo kwa jina lake mwenyewe nayo inaitwa mnara wa Absalomu hata hivi leo.
Tumepatana mimi nawe, na baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea zawadi, fedha na dhahabu; basi nenda, uyavunje mapatano yako na Baasha mfalme wa Israeli, ili aache mashambulizi juu yangu.
Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya,
na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi;
Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.
Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la BWANA.
Makaburi ni nyumba zao hata milele, Maskani zao vizazi hata vizazi. Japo waliwahi kuyamiliki mashamba, Kwa majina yao wenyewe.
Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabibu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa upendo wangu.
Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu kuhusu shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana;
Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe makao yangu ya kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?