Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Mhubiri 12:3 - Swahili Revised Union Version

Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka; Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha; Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba; Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wakati ambapo mikono inayokulinda inatetemeka, miguu yako imara imepindika, meno yako ya kusagia hayafai kwa uchache, na macho ya kuchungulia dirishani yamefifia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wakati ambapo mikono inayokulinda inatetemeka, miguu yako imara imepindika, meno yako ya kusagia hayafai kwa uchache, na macho ya kuchungulia dirishani yamefifia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wakati ambapo mikono inayokulinda inatetemeka, miguu yako imara imepindika, meno yako ya kusagia hayafai kwa uchache, na macho ya kuchungulia dirishani yamefifia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka, nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha, wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache, nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka, nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha, wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache, nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka; Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha; Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba; Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

Tazama sura
Tafsiri zingine

Mhubiri 12:3
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.

Na macho ya Israeli yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona vizuri. Akawaleta kwake, naye akawabusu, na kuwakumbatia.

Amezipunguza nguvu zangu njiani; Amezifupisha siku zangu.

Nilisikitika kana kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Niliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.

Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza.

BWANA wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu akiwa ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana.

Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),