Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
Methali 8:12 - Swahili Revised Union Version Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi Hekima ninao ujuzi; ninayo maarifa na busara. Biblia Habari Njema - BHND Mimi Hekima ninao ujuzi; ninayo maarifa na busara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi Hekima ninao ujuzi; ninayo maarifa na busara. Neno: Bibilia Takatifu “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara. Neno: Maandiko Matakatifu “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara. BIBLIA KISWAHILI Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa makao yangu; Natafuta maarifa na busara. |
Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
na mfano wa yote aliyokuwa nao rohoni, kuhusu nyua za nyumba ya BWANA, na ya vyumba vyote vilivyoizunguka, ya hazina za nyumba ya Mungu, na ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu;
Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa BWANA, naam, kazi zote za mfano huu.
Na Yuda walipotazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia BWANA, na makuhani wakapiga parapanda.
Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa viumbe wako.
Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda;
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;