Methali 5:15 - Swahili Revised Union Version Unywe maji ya tangi lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Kunywa maji kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kisima chako mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Unywe maji ya tangi lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. |
Bustani iliyofungwa ni dada yangu, bibi arusi, Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa mhuri.
Msimsikilize Hezekia; maana mfalme wa Ashuru asema hivi, Fanyeni suluhu na mimi, mkatoke mnijie, mkale kila mtu matunda ya mzabibu wake na matunda ya mtini wake, mkanywe kila mmoja maji ya kisima chake mwenyewe;
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.