Methali 5:11 - Swahili Revised Union Version Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Biblia Habari Njema - BHND Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza wakati mwili wako utakapoangamizwa. Neno: Bibilia Takatifu Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. Neno: Maandiko Matakatifu Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. BIBLIA KISWAHILI Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; |
Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?
Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji, ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosea mumewe, hayo maji yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu wake.
Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.
Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.