Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde popote; ujiponye mlimani, usije ukaangamia.
Methali 28:22 - Swahili Revised Union Version Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu bahili hukimbilia mali, wala hajui kwamba ufukara utamjia. Biblia Habari Njema - BHND Mtu bahili hukimbilia mali, wala hajui kwamba ufukara utamjia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu bahili hukimbilia mali, wala hajui kwamba ufukara utamjia. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, naye hana habari kuwa umaskini unamngojea. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, naye hana habari kuwa umaskini unamngojea. BIBLIA KISWAHILI Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjia. |
Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde popote; ujiponye mlimani, usije ukaangamia.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu.