Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.
Methali 23:3 - Swahili Revised Union Version Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usitamani vyakula vyake vizuri, maana vyaweza kukudanganya. Biblia Habari Njema - BHND Usitamani vyakula vyake vizuri, maana vyaweza kukudanganya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usitamani vyakula vyake vizuri, maana vyaweza kukudanganya. Neno: Bibilia Takatifu Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. Neno: Maandiko Matakatifu Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. BIBLIA KISWAHILI Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila. |
Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.
Huyo mfalme akawaagizia wapewe chakula kama cha mfalme, na divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.
Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
mvue mwenendo wenu wa kwanza, utu wa zamani unaoharibika, kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;