Methali 23:18 - Swahili Revised Union Version Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakika kuna kesho ya milele, na tumaini lako halitakuwa bure. Biblia Habari Njema - BHND Hakika kuna kesho ya milele, na tumaini lako halitakuwa bure. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakika kuna kesho ya milele, na tumaini lako halitakuwa bure. Neno: Bibilia Takatifu Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali. Neno: Maandiko Matakatifu Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali. BIBLIA KISWAHILI Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. |
Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Na mwanadamu atasema, Hakika iko thawabu yake mwenye haki. Hakika yuko Mungu Anayehukumu katika dunia.
Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
Abrahamu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo yako mema katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unateseka.
kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama sikuzote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu.