Methali 2:8 - Swahili Revised Union Version Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Biblia Habari Njema - BHND Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huilinda mienendo ya watu watendao haki, na kuzihifadhi njia za waaminifu wake. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. BIBLIA KISWAHILI Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake. |
Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.
Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako.
Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;
Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;