Methali 2:13 - Swahili Revised Union Version Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; Biblia Habari Njema - BHND watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza watu waziachao njia nyofu, ili kuziendea njia za giza; Neno: Bibilia Takatifu wale wanaoacha mapito ya unyoofu, wakatembea katika njia za giza, Neno: Maandiko Matakatifu wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza, BIBLIA KISWAHILI Watu waziachao njia za unyofu, Ili kuziendea njia za giza; |
Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika mienendo yao; wamejifanyia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.
Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa.
na hao waliorudi nyuma, na kuacha kumfuata BWANA; na hao wasiomtafuta BWANA, wala kumwulizia.
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.