Ndipo mtu aliye kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.
Mathayo 9:32 - Swahili Revised Union Version Na hao walipokuwa wakiondoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Biblia Habari Njema - BHND Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Neno: Bibilia Takatifu Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa. BIBLIA KISWAHILI Na hao walipokuwa wakiondoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. |
Ndipo mtu aliye kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, watu wakastaajabu.