Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
Mathayo 6:11 - Swahili Revised Union Version Utupe leo riziki yetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utupe leo chakula chetu cha kila siku. Biblia Habari Njema - BHND Utupe leo chakula chetu cha kila siku. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utupe leo chakula chetu cha kila siku. Neno: Bibilia Takatifu Utupatie riziki yetu ya kila siku. Neno: Maandiko Matakatifu Utupatie riziki yetu ya kila siku. BIBLIA KISWAHILI Utupe leo riziki yetu. |
Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Basi tunawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.
Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana akiwa katika nchi ya Moabu alipata habari kuwa BWANA alikuwa amewajia watu wake na kuwapa chakula.