Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
Mathayo 4:25 - Swahili Revised Union Version Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Yudea, na ng'ambo ya Yordani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ngambo ya mto Yordani, yalimfuata. Biblia Habari Njema - BHND Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ngambo ya mto Yordani, yalimfuata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng'ambo ya mto Yordani, yalimfuata. Neno: Bibilia Takatifu Makundi makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea, na kutoka ng’ambo ya Yordani. Neno: Maandiko Matakatifu Makutano makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Uyahudi na kutoka ng’ambo ya Mto Yordani. BIBLIA KISWAHILI Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Yudea, na ng'ambo ya Yordani. |
Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa,
Naye alipowaona makundi ya watu, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;
Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka ziwa la Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Yudea wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao;
Na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.