(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya.
Mathayo 4:15 - Swahili Revised Union Version Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ngambo ya mto Yordani, Galilaya, nchi ya watu wa mataifa! Biblia Habari Njema - BHND “Nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ngambo ya mto Yordani, Galilaya, nchi ya watu wa mataifa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng'ambo ya mto Yordani, Galilaya, nchi ya watu wa mataifa! Neno: Bibilia Takatifu “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya Mataifa: Neno: Maandiko Matakatifu “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya kuelekea baharini, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya watu wa Mataifa: BIBLIA KISWAHILI Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, |
(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya.
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo awali aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa.
akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Yudea, na ng'ambo ya Yordani.
Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Nao wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya vilima ya Yuda.
Tena katika kabila la Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na mbuga zake za malisho, na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho; miji mitatu.