Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;
Mathayo 27:27 - Swahili Revised Union Version Ndipo askari wa mtawala wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima. Biblia Habari Njema - BHND Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima. Neno: Bibilia Takatifu Kisha askari wa mtawala wakampeleka Isa kwenye Praitorio, na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha askari wa mtawala wakampeleka Isa kwenye Praitorio na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. BIBLIA KISWAHILI Ndipo askari wa mtawala wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima. |
Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;
Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.
Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.
Basi ilipoamriwa tuabiri hadi Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya ofisa mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.