Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.
Mathayo 27:25 - Swahili Revised Union Version Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!” Biblia Habari Njema - BHND Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!” Neno: Bibilia Takatifu Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!” Neno: Maandiko Matakatifu Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!” BIBLIA KISWAHILI Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. |
Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.
Naye BWANA atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga.
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande; naye yeyote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
Walipopingana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.
akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.
Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua;
isije ikamwagika damu ya asiye makosa kati ya nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, ikawa na damu juu yako.
Jicho lako lisimhurumie, lakini uondoe damu ya asiye makosa katika Israeli, ili upate kufanikiwa.
Itakuwa mtu awaye yote atakayetoka katika mlango wa nyumba yako kwenda njiani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, na sisi tutakuwa hatuna hatia; na mtu atakayekuwa ndani ya nyumba yako damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu, mkono wa mtu ukimpata.