Lakini kuhusu siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Mathayo 24:42 - Swahili Revised Union Version Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Neno: Bibilia Takatifu “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. Neno: Maandiko Matakatifu “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana Mungu wenu. BIBLIA KISWAHILI Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. |
Lakini kuhusu siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliujua ule wakati mwizi atakaokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyotazamia Mwana wa Adamu yuaja.
Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu uko karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.
(Tazama, naja kama mwizi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)