Mathayo 23:32 - Swahili Revised Union Version Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza! Biblia Habari Njema - BHND Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza! Neno: Bibilia Takatifu Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu! Neno: Maandiko Matakatifu Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu! BIBLIA KISWAHILI Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. |
wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;
Lakini hawakunisikiliza, wala kutega sikio lao; bali walifanya shingo yao kuwa ngumu; walitenda mabaya kuliko baba zao.
Na tazama, ninyi kizazi cha watu wenye dhambi, mmeinuka badala ya baba zenu ili kuongeza tena hizo hasira kali za BWANA juu ya Israeli.
huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho.