Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huku na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.
Mathayo 22:9 - Swahili Revised Union Version Basi Nendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje harusini.’ Biblia Habari Njema - BHND Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje harusini.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje harusini.’ Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ BIBLIA KISWAHILI Basi Nendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni harusini. |
Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huku na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.
Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia, katika siku ya dhiki.
Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, nanyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.
Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.
na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.