Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.
Mathayo 21:6 - Swahili Revised Union Version Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, wale wanafunzi walikwenda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, wale wanafunzi walikwenda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, wale wanafunzi walikwenda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza. Neno: Bibilia Takatifu Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Isa alivyokuwa amewaagiza. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Isa alivyokuwa amewaagiza. BIBLIA KISWAHILI Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, |
Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.
Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.
Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nilitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao.
Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwanapunda, mtoto wa punda.
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.