Mathayo 20:4 - Swahili Revised Union Version na hao nao akawaambia, Nendeni nanyi pia katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akawaambia, ‘Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu, nami nitawapeni haki yenu.’ Biblia Habari Njema - BHND Akawaambia, ‘Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu, nami nitawapeni haki yenu.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akawaambia, ‘Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu, nami nitawapeni haki yenu.’ Neno: Bibilia Takatifu Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’ Neno: Maandiko Matakatifu Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’ BIBLIA KISWAHILI na hao nao akawaambia, Nendeni nanyi pia katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. |
Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.
Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
Ninyi akina bwana, wapeni watumishi wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyasisitizie sana, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Mambo hayo ni mazuri sana, tena yana manufaa kwa wanadamu.
Kwa hiyo iweni tayari, na makini; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.