Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 20:27 - Swahili Revised Union Version na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu. Biblia Habari Njema - BHND na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu. Neno: Bibilia Takatifu naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu: Neno: Maandiko Matakatifu naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu: BIBLIA KISWAHILI na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; |
Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;
kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye.
Nami nitakuwa radhi kutumia na kutumiwa kwa ajili yenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?
Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.