Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Mathayo 19:19 - Swahili Revised Union Version Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waheshimu baba yako na mama yako; na, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” Biblia Habari Njema - BHND Waheshimu baba yako na mama yako; na, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waheshimu baba yako na mama yako; na, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” Neno: Bibilia Takatifu waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.” Neno: Maandiko Matakatifu waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.” BIBLIA KISWAHILI Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. |
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.
Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA.
Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.