Mathayo 18:22 - Swahili Revised Union Version Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba. Biblia Habari Njema - BHND Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba. Neno: Bibilia Takatifu Isa akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. BIBLIA KISWAHILI Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. |
Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.
Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.
Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matusi yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;
mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.