Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
Mathayo 15:21 - Swahili Revised Union Version Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliondoka mahali hapo akaenda kukaa katika sehemu za Tiro na Sidoni. Neno: Bibilia Takatifu Isa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. Neno: Maandiko Matakatifu Isa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. BIBLIA KISWAHILI Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. |
Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.
BWANA akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza mpaka kufikia Sidoni ulio mkuu, tena hadi kufika Misrefoth-maimu, tena hata kufikia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawaua wote, wasibakize hata mtu mmoja
na watu wote wenye kukaa nchi za vilima kutoka Lebanoni hadi Misrefoth-maimu, maana, hao Wasidoni wote; hao wote nitawafukuza watoke mbele ya wana wa Israeli; lakini wewe uwape Israeli kuwa ni urithi wao, kama nilivyokuamuru.
Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu;