Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Mathayo 12:8 - Swahili Revised Union Version Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Mwana wa Mtu ana uwezo juu ya Sabato.” Biblia Habari Njema - BHND Maana Mwana wa Mtu ana uwezo juu ya Sabato.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana Mwana wa Mtu ana uwezo juu ya Sabato.” Neno: Bibilia Takatifu kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” BIBLIA KISWAHILI Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato. |
Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.
Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Inuka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
Kwa wale wasio na sheria nilikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
Nilikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,