Mathayo 12:19 - Swahili Revised Union Version Hatateta wala hatapaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika barabarani. Biblia Habari Njema - BHND Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika barabarani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika barabarani. Neno: Bibilia Takatifu Hatagombana wala kupaza sauti, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani. Neno: Maandiko Matakatifu Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani. BIBLIA KISWAHILI Hatateta wala hatapaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani. |
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hadi ailetapo hukumu ikashinda.
Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu;